BENDI za Mashujaa na Mashauzi Classic
zitatumbuiza kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta mrembo wa Tabata, Miss Tabata
2012 kitakachofanyika Juni Mosi katika ukumbi wa Da West Park,
Tabata.
Akizungumza jana, mratibu wa shindano
hilo, Godfrey Kalinga, alisema kuwa wameamua kuweka burudani nyingi yenye ladha
tofauti ili kukidhi kiu ya rika zote watakaohudhuria shindano hilo ambalo ni
kivutio kwa wakazi jijini.
Kalinga alisema shindano hilo pia
litatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa shindano la
Miss Tabata.
“Shindano la mwaka huu litakuwa ni la aina
yake kwa sababu hii utakuwa ni mwaka wetu wa 10 tangua kuanza kuandaa Miss
Tabata ndio maana tunaleta burudani nyingi,” alisema mratibu huyo wa Bob
Entertainment na Keen Arts.
Alisema warembo waliyowahi kushinda mataji
mbalimbali ya shindano hilo, pia wamealikwa kusherehekea miaka 10 ya Miss
Tabata.
Shindano hili limedhaminiwa na Dodoma
Wine, Redds, Integrated Communications, Fredito Entertainment, Multichoice
Tanzania, Screen Masters, Kitwe General Traders, Step In Electronics, Brake
Point, Atriums Hotel na Lady Pepeta.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano
wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Dar West Park.
Warembo hao ni Neema Saleh (18), Noella
Michael (19), Queen Issa (20), Hycalisa Joseph (18), Phillios Lemi (19),
Wikllihemina Mvungi (20) na Nightness Rajab (19).
Wengine ni Suzanne Pancras (19), Caroline
David (21), Khadija Nurdin (19), Jamila Omary (18), Advent Mamkwe
(21), Nadya Marjeby (21), Axer Peter (20), Rahama Hassan (19), Mercy Mlay (21)
na Diana Simon Laizer (20).
Warembo 10 watachaguliwa kushiriki
mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata kwa
sasa ni Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya
vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi
alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds.
Katika shindano la mwaka juzi Juliet
William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
Juliet ndiye anayeshikilia taji la dunia
la Miss Progressive International.