HATIMAYE kilio cha muda mrefu cha waandaji wa tamasha
la filamu za nchi za majahazi (ZIFF) kimesikika baada ya Kampuni ya ving’amuzi
ya Television ya kulipia ZUKU kuamua kulidhamini
kwa sh bil 1 kwa kipindi cha miaka 10.
Katika taarifa iliyotolewa juzi jijini Dar es
Salaam ilisema kuwa ZUKU inalidhamini
tamasha hilo kwa nia ya kutaka kulifanya liwe la kimataifa na la kwanza kuliko
tamasha lolote lile Afrika Mashariki ba Kati na Afrika kwa ujumla.
Mkurugenzi Mkuu wa Wananchi Group, inayomiliki
ZUKU, Richard Bell alisema hiyo ni hatua
kubwa katika kukuza ushirikiano uliopo kati ya ZUKU na ZIFF na kwamba utainua
na kustawisha sanaa hapa nchini na kupanua wigo wa filamu.
“Tumedhamiria kulifanya tamasha hili kutambulika
kote Duniani, kadiri linavyokuwa ndivyo tutakavyozidi kuliongezea uwezo huu ni
mwanzo tu,” alisema Bell.
Bell pia aliwaomba wadau wengine kujumuika na
ZIFF, kudhamini sambamba na kujitangaza
zaidi kwani milango ipo wazi kwa kila mdau kwa sasa na baadae kujitokeza.
Aidha, Mwenyekiti wa ZIFF, Mahmoud Thabit Kombo, aliwashukuru ZUKU kwa
udhamini huo ambapo alisema ZIFF ni kiungo na chombo muhimu cha utamaduni wa
Mwafrika na kila mmoja anapaswa kujivunia.
Udhamini huo wa miaka 10 utaishia mwaka 2022 na
Mwenyekiti huyo anaamini kuwa hadi hapo ZIFF itakuwa imejenga uwezo mkubwa na
mahusiano ya kudumu na taasisi mbalimbali za biashara na za habari.
Tamasha la ZIFF linatarajiwa kufanyika huko Ngome
kongwe Zanzibar kuanzia Julai 7 hadi 15,
mwaka huu, ambapo vikundi mbali mbali vya sanaa