LAMAR KUSIMAMIA KAZI ZA MR.NICE


HATIMAYE kilio cha muda mrefu cha waandaji wa tamasha la filamu za nchi za majahazi (ZIFF) kimesikika baada ya Kampuni ya ving’amuzi ya Television ya kulipia ZUKU  kuamua kulidhamini kwa sh bil 1 kwa kipindi cha miaka 10.

Katika taarifa iliyotolewa juzi jijini Dar es Salaam ilisema kuwa  ZUKU inalidhamini tamasha hilo kwa nia ya kutaka kulifanya liwe la kimataifa na la kwanza kuliko tamasha lolote lile Afrika Mashariki ba Kati na Afrika kwa ujumla.

Mkurugenzi Mkuu wa Wananchi Group, inayomiliki ZUKU,  Richard Bell alisema hiyo ni hatua kubwa katika kukuza ushirikiano uliopo kati ya ZUKU na ZIFF na kwamba utainua na kustawisha sanaa hapa nchini na kupanua wigo wa filamu.

“Tumedhamiria kulifanya tamasha hili kutambulika kote Duniani, kadiri linavyokuwa ndivyo tutakavyozidi kuliongezea uwezo huu ni mwanzo tu,” alisema Bell.

Bell pia aliwaomba wadau wengine kujumuika na ZIFF,  kudhamini sambamba na kujitangaza zaidi kwani milango ipo wazi kwa kila mdau kwa sasa na baadae kujitokeza.

Aidha, Mwenyekiti wa ZIFF,  Mahmoud Thabit Kombo, aliwashukuru ZUKU kwa udhamini huo ambapo alisema ZIFF ni kiungo na chombo muhimu cha utamaduni wa Mwafrika  na kila mmoja anapaswa kujivunia.

Udhamini huo wa miaka 10 utaishia mwaka 2022 na Mwenyekiti huyo anaamini kuwa hadi hapo ZIFF itakuwa imejenga uwezo mkubwa na mahusiano ya kudumu na taasisi mbalimbali za biashara na za habari.

Tamasha la ZIFF linatarajiwa kufanyika huko Ngome kongwe  Zanzibar kuanzia Julai 7 hadi 15, mwaka huu, ambapo vikundi mbali mbali vya sanaa vitashiriki na filamu mbali mbali zitaoneshwa.



Mwisho



Lamar kuisambaza albamu ya Mr. Nice

Na Ruhazi Ruhazi



MTAYARISHAJI mahiri wa muziki nchini Lamar Niekamp maarufu kama Lamar, amesema ataisimamia na kuiingia sokoni kazi mpya ya Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ iitwayo ‘Tabia Gani’.
Lamar alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana kushindwa kuvumulia mlolongo mrefu kutoka kwa wasambazaji.
Alisema kuwa wamepanga kuiingiza sokoni albamu hiyo ya ‘Tabia Gani’, ambyo pia ina nyimbo za ‘Maneno Maneno’, ‘Nionaje’, ‘Ulisemaje’, ‘Amini’, ‘Mfalme’ na ‘Kupata’.
“Kaka tumeamua albamu mpya ya Mr. Nice tuiingize sokoni na kuisambaza wenyewe, nadhani kuanzia wikiendi  hii tutaiingiza sokoni,” alisema Lamar.
Mr. Nice aliyepata kutamba vilivyo kwa miondoko yake ya Takeu, amewashirikisha wasanii mbali mbali, katika albamu hiyo mpya, inayovunja ukimya wake wa miaka saba

1 Comments

  1. I have read so many posts about the blogger lovers but this piece of writing is really
    a fastidious piece of writing, keep it up.
    Also visit my web site ; gerber life insurance co

    ReplyDelete
Previous Post Next Post