SIMBA YAFA 'KIUME' SUDAN

SIMBA SC imeshindwa kutimiza ndoto za kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kutolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly Shandy ya Sudan kufuatia sare ya jumla ya tatu. Katika mchezo huo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shandi, penalti za Shandy zilifungwa na Razak Yakubu, Orwa, Bashir, Saddam, Isaac Seun Malik, Faris Abdallah, Fareed Mohamed Zakaria Nasu na kipa Abdulrahman Ali. Waliofunga penalti za Simba ni Felix Sunzu, Salum Machaku, Emanuel Okwi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Victor Costa, Mwinyi Kazimoto na Amir Maftah. Eltigani alikosa kwa upoande wa Shandy wakati Mafisango na Kaseja walikosa. Aliyeihakikishia Simba kutpolewa alikuwa ni Nahodha Kaseja, ambaye alikosa penalti ya 10. Shandy waliingia kwenye mchezo wa leo, wakiwa nyuma kwa 3-0 kutokana na ujshindi wa SImba kwenye mechi ya kwanza, Dar es Salaam. Hadi mapumziko, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake na hiyo ilijenga matumaini kwamba, SImba itasonga mbele, lakini kipindi cha pili mambo yalibadilika mno. Mabao mawili ya Fareed Mohamed katika za 46 na 64 na lingine la Hamouda Bashir dakika ya 50, yaliisaidia Al Ahly Shandy kushinda 3-0 na kufanya sare ya jumla ya 3-3, baada ya dakika 180 za mechi mbili. Lawama zote zimuendee beki Victor Costa kwa kufungisha mabao mawili- hususan la pili na la tatu ambalo dhahiri yalitokana na ‘ubishoo’ wake usio na maana. Hii inahidhirisha mchezaji huyo aliyepangwa kwa dharula leo, kocha Milovan Cirkovick alikuwa hakosei kutompanga- kwani leo ameigharimu timu na haijulikani kwa nini apangwe yeye badala ya Obadia Mungusa.

1 Comments

  1. Wamekufa kiume nini, tokeni hapa tutanza kusikia ha, ha, hujuma, sasa ni Victor Costa...soccer la bongo bwana...poleni sana, ndiyo mpira huo.
    Mdau
    Washington

    ReplyDelete
Previous Post Next Post