Tullo kulia akiwa na mamapipiro
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
kinatoa pongezi kwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Tanzania Daima,
Tullo Chambo kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha
Riadha Tanzania
(RT).
Chambo alitwaa nafasi hiyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa RT
uliofanyika Jumapili mjini Morogoro, ambapo ni miongoni mwa wajumbe wapya
walioingia kwenye chama hicho.
Wengine walioshinda ni Anthony Mtaka ambaye anakuwa Rais
mpya wa RT, wakati Makamu wa Rais Utawala ni William Kallaghe, Makamu wa Rais
Ufundi, Dk. Ahmed Ndee, Katibu Mkuu, Suleiman Nyambui, Katibu Msaidizi, Ombeni
Zavalla, Mhazini, Is-Haq Suleiman.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mwinga Mwanjala, Meta
Petro, Peter Mwita, Rehema Killo, Lwiza John, Zakaria Barrie, Zakaria Gwanda,
Robert Kalyahe na Christian Matembo.
TASWA inatambua Chambo ni mwanahabari mzoefu, ambaye kwa
muda mrefu amekuwa mhariri wa habari za michezo na ni mtu mwenye kujua mambo
mengi yanayohusu riadha, hivyo atakuwa kiungo muhimu kwa watu wa riadha, pia
atakuwa kiongo kizuri kwa waandishi wa habari za michezo kuhusiana na mambo ya
riadha.
TASWA inaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kadri
itakavyoweza na inamtakia kila la heri, huku ikiamini hatawaangusha Wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa RT waliomuamini wakamchagua kushika wadhifa huo.
Pia Taswa inawapongeza viongozi wote wa RT walioingia
madarakani Jumapili, ikiamini watakuwa chachu ya mafanikio ya riadha hapa
nchini.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
25/05/2012