BINGWA wa
dunia wa ndondi WBF Francis Cheka amewasili mjini Dodoma leo ambapo kesho atatambulishwa
rasmi bungeni sambamba na kupongezwa.
Cheka
aliyetwaa ubingwa huo ijumaa iliyopita baada ya kumtwanga Mmarekani Phil
Williams, amekwenda Dodoma kwa mwaliko wa Waziri wa habari utamaduni, Vijana na
Michezo Dk.Fenella Mukangara.