WAZEE YANGA WAMTIMUA KATIBU MKUU MPYA

BARAZA la wazee wa klabu ya Yanga leo wamtimua Katibu mkuu mpya aliyeajiriwa ndani ya klabu hiyo kurithi mikoba ya Lawrance Mwalusako ambaye mkataba wake umemalizika.
Katibu Mkuu wa Baraza hilo Ibrahim Akilimali (pichani)amesema kwamba wameamua kumtimua mtendaji huyo raia wa Kenya baada ya kutokuwa na taarifa juu ya ujio wake mkitu ambacho ni kinyume nba katiba ya klabu hiyo.
Alisema kabla ya kumtimua walimuhoji alipotokea lakini alishindwa kueleza ameletwa hapo na nani na hasa ikizingatiwa kuwa si raia wa Tanzania, pia si mwanachama wa Yanga hali ambayo ilizidi kuwatia mashaka.
"Kwa kweli tulimuona huyu mtu ni kama mbambaishaji na mwenye lengo la kutaka kuja kuiba rasilimali za kalbu kwani si raia na pia si mwanachama wa Yanga, hata hivyo sisi kama baraza la Wazee hatuna taarifa juu yake,"alisema

Post a Comment

Previous Post Next Post