TIMU za Azam
Fc na Ashanti United zinazoshiriki Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kesho
zitamenyana katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu utakaofanyika katika
dimba la Chamazi Complex.
Msemaji wa
Azam Fc iliyoandaa mchezo huo, Jaffer Iddy amesema leo kwamba mchezo huo ni
maalum kwa kuzipima nguvu timu hizo ambazo kwa sasa zipo katika mapumziko
mafupi ya ligi hiyo.
Alisema
mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 jioni hautakuwa na kiingilio hivyo
amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Kwa upande
mwingine, Maganga amesema kwamba wachezaji wake waliokuwa majeruhi John Bocco ‘Adebayor’
na Aggrey Morris hali zao zimeimarika na tayari wameanza mazoezi mepesi.