KESHO
Ijumaa, Septemba 6 mwaka 2013, klabu ya Simba itacheza mechi ya kirafiki na
mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Zanzibar, KMKM, katika mechi itakayochezwa
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Lengo
kuu la mechi hiyo ni mazoezi kwa Simba ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya
Mtibwa Sugar uliopangwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu.
Kikosi
kamili cha KMKM kimewasili jijini Dar es Salaam tayari na leo saa tano na nusu
kamili nahodha wake, Abdi Kassim Babi na kocha mkuu wa timu hiyo wanatarajiwa
kuzungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa City Lounge katikati ya
jiji.
Simba
inaendelea na mazoezi yake jijini na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri
na tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
Mechi
hiyo itaanza majira ya saa 11 jioni ili kuwezesha watu wengi kwenda uwanjani
kutazama mechi hiyo ikizingatiwa kuwa Ijumaa ni siku ya kazi.
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
EEE