|
Burudani ya mabinti |
|
Tenga na Mgongolwa wakifurahia |
|
Tenga na Mgongolwa |
|
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kushoto, katikati mama Juliana Yassoda na kulia Robin |
|
Wadau wa soka, Msafiri Mgoyi Mjumbe wa TFF, beki wa zamani Taifa Stars na Meneja wa timu hiyo, Leopold Mukebezi, Fred na kocha Joseph Kanakamfumu |
|
Mwandishi wa Nipashe Somoe Ng'itu na kocha Jamhuri Kihwelo |
|
Makamu wa kwanza wa rais wa TFF, Athumani Nyamlani na Mdau Salim |
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), jioni hii imeingia mkataba wa kuidhamini timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wa miaka mitano, wenye thamani ya Sh. Bilioni 23.
Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Kempinski, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wote wakuu wa TFF, TBL na wadau mbalimbali.
Stars, ambayo tangu mwaka 2006, ilikuwa ikidhaminiwa na kampuni nyingine ya Bia Tanzania, Serengeti (SBL) sasa itakuwa ikivaa jezi zenye nembo ya bia ya Kilimanjaro, ambayo pia ni wadhamini wa Simba na Yanga.
Rais wa TFF, Leodegar Chillah Tenga alitiliana saini mkataba huo na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche katika hafla iliyopambwa na burudani nyepesi nyepesi.
Katika hafla hiyo liyofana, utiaji saini wa mkataba huo, ulishuhudiwa na mawakili wa pande zote mbili, TFF ikiwakilishwa na Alex Mgongolwa.
SOURCE: BIN ZUBEIRY (http/bongostaz.blogspot.com)