Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana Mei 2 mwaka huu kujadili rufani
iliyowasilishwa mbele yake na klabu ya African Lyon.
Klabu hiyo ya Ligi Kuu
inailalamikia TFF ikipinga uamuzi uliofanywa na Kamati yake ya Ligi juu ya
kuvunjika kwa pambano la ligi hiyo kati ya Azam na Mtibwa Sugar lililochezwa
hivi karibuni kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Katika rufani yake, Lyon
imedai uamuzi uliofanywa na Kamati ya Ligi ya TFF haikuwa sahihi, kwani
haukuzingatia kanuni za ligi hiyo kuhusu timu inayogomea mchezo.
Kamati hiyo chini ya Kamishna
Mstaafu wa Polisi, Alfred Tibaigana inatarajia kufanya kikao chake kuanzia 8
mchana.