Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) itacheza na Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika
Mei 12 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam .
Twiga Stars hivi iko katika ziara ya mechi za kirafiki
katika mikoa ya Dodoma
na Mwanza. Leo (Mei 8 mwaka huu) itacheza na kombaini ya Mkoa wa Dodoma ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 katika
mchezo utakaofanyika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma .
Kesho (Mei 9 mwaka huu) itaondoka kwenda jijini Mwanza ambapo
pia itacheza mechi moja ya kirafiki Mei 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba, na kurejea Dar es Salaam tayari kwa
ajili ya mechi dhidi ya Zimbabwe .