Mabao ya Dodoma
katika mechi hiyo ya kundi C yalifungwa na Japhet Lunyungu dakika ya 59 wakati
Frank Kaji aliwahakikishia ushindi washindi dakika saba kabla ya filimbi ya
mwisho baada ya kupachika bao la pili.
Nayo Mjini Magharibi iliifunga Iringa mabao 3-0 katika mechi
ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
Mechi za asubuhi zilizokuwa zichezwe leo kati ya Arusha na
Kusini Pemba kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers na Pwani na Tabora kwenye
Uwanja wa Karume sasa zitachezwa kuanzia saa 8 mchana kutokana na kutokuwepo
mawasiliano ya barabara asubuhi (Morogoro
Road ) kutoka mkoani Pwani kuingia Dar es Salaam.
Leo jioni kutakuwa na mechi kati ya Rukwa na Ruvuma (Tanganyika Packers), Mwanza na Tanga (Nyumbu),
Kaskazini Unguja na Mara (Tamco) na Singida na Kagera (Karume).