MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umesogeza mbele
tamasha la Watani wa Jadi lililokuwa
lifanyike 1/7/2012 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi Sikukuu ya Iddi Mosi
ambayo inatarajiwa kuwa 21 au 22 Agosti mwaka huu.
Tamasha hilo
ambalo linawakutanisha Timu ya Simba Veteran na Yanga Veteran pia kutakuwa
mchezo wa mieleka kati ya msanii wa filamu, Lumole Matovolwa (Big) na Roman
Mng’ande (Romario) wa Msondo wanawake watakaopambana katika mieleka ni Mwajuma
Jimama na Sophia Lubuva kutakuwa na Ngongoti Basketball.
Vikundi maarufu vya ushangiliaji Mpira
Pesa cha Simba na Yanga Bomba (Yanga)
vitapambana katika mchezo wa soka na baadaye kushangilia timu zao zikimenyana
na bendi ya Msondo Music Band itatumbuiza.
Limeosogezwa
mbele ili kutoa nafasi ya kutosha kwa ajili ya maandalizi ya timu za Simba na
Yanga Veteran ambazo zitapambana siku hiyo, pia kutoa nafasi kwa mashabiki na
watoto wengi zaidi kuweza kuhudhuria.
Pia filamu
iliyochezwa na SHIWATA ya Kisufuria itazinduliwa. iliyowashirikisha wasanii maarufu
kama Ahmed Olotu (Mzee Chilo), Big, Nisha,
Haji Mboto na Mama Mau.
Madhumuni ya
Tamasha hilo ni
kukusanya fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Wasanii na Waandishi wa
Habari, zinazojengwa katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga ambazo mpaka sasa
nyumba tano (5) za kisasa zimejengwa.
Mwenyekiti wa
SHIWATA,Cassim Taalib alisema kiongozi
wa Yanga Veteran Bakari Malima (Jembe Ulaya) na kiongozi wa Simba Thomas Kipese
wametamba kuonesha kazi siku hiyo.
Kipese akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema
kuahirishwa kwa mpambano wao kunawapa nafasi wachezaji wake kujiandaa vizuri
kwa mazoezi, naye Malima alisema wachezaji wake wako fiti wakati wote
watakapohitajika kuingia uwanjani watashinda pambano hilo .
Wachezaji wa
Simba wanajiandaa na pambano hilo
ni Madaraka Suleiman, Abdul Mashine, Barnabas Sekelo, Said Kokoo, Boniface
Pawasa,Duwa Said, Mrisho Moshi,
Kamba Lufo, Malota Soma, Shabani Kisiga, Abubakar Kombo, Iddi seleman,
Majuto Komu, Ramdhani Waso, Kelvin Mhagama, Issa Manofu na Kipese.
Nao wachezaji wa Yanga wanajiandaa na pambano hilo ni
Peter Manyika, Mzee Abdallah, Anwar Awadh, Kenny Mkapa, Salvatory Edward,
Shabani Ramadhani, Abdul Maneno, Steven Nyenge, Mohamed Hussen (Mmachinga),
Edibilly Lwinyamila, Sekilojo Chambua, Thabit Bushako, Ally Mayay, Banza
Tshikala na Malima.