Bendi dansi ya FM maarufu
kama wazee WANGWASUMA pamoja na msanii
wa vichekesho MPOKI watatoa burudani ya anina yake katika shindano la kumsaka
malkia wa kitongoji cha Kigamboni City
2012' litakalofanyika Juni 15 mwaka huu
katika ukumbi wa Navy Beach ulioko huko
Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, bendi ya FM inafahamika kwa kutoa burudani nzuri kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini .
Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, bendi ya FM inafahamika kwa kutoa burudani nzuri kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini .
Kuhusiana na msanii MPOKI, SOMOE amesema kuwa mchekeshaji
huyo ambaye pia ni mkazi wa KIGAMBONI amekuwa ni kati ya waburudishaji katika
sanaa ya uchekeshaji na kupendwa na watu wa rika zote hivyo mashabiki wa urembo
wataweza kupata burudani ya uhakika .
Mratibu huyo kutoka kampuni ya K& L, alisema kuwa Jumla ya warembo 15 wanaendelea kujifua katika
kambi ya mazoezi chini ya mwalimu wao miss TEMEKE HAWA ISMAIL ambaye
anashirikiana na mshiriki wa miss TANZANIA mwaka jana BLESSING NGOWI.
Amewataja warembo hao kuwa ni pamoja na CAROLYNE
DANDU,FATINA FRANSIS,EDDA SLYVESTER,AISHA MUSSA,ROSEMARY PETER,DOREEN
KWEKA,CAROLINE PETER,AGNES GOODLUCK,SOPHIA MARTINE,ROSEMARY DEOGRATIUS,BEATRICE
BONIFACE,JULIETH PHILIP na KHADIJA KOMBO.
"Kigamboni ni zaidi ya kitongoji, tunaamini shindano letu litakuwa na mvuto na hadhi ya kipekee kama eneo lake lilivyo," aliongeza.
Alisema kuwa warembo watakaofanya vizuri watapata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika mashindano ya kanda ambayo yatafanyika baadaye mwaka huu.
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF,Hope country Motel,Norbro’s Collections,Screen masters,Global Publishers.