Malkia wa mipasho na mshindi wa tuzo za Tanzania Kili music
Awards 2012 Khadija Kopa anategemewa kuwa kivuto kikubwa kwa kutoa burudani ya
kipekee katika shindano la kumsaka mlimbwende wa MISS lAKE ZONE INTERCOLLEGES
2012 ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika mkoani Kagera katika mji wa Bukoba.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hii jijini Dar es salaam Mwandaaji wa shindano hilo
Bw.Joseph Rwebangira amesema kuwa asilimia kubwa ya maandalizi
yameshatimia,hata hivyo Rwebangira aliongezea kuwa mshereheshaji wa siku hiyo
atakuwa mchekeshaji maarufu afrika mashariki na kati Mpoki wa the origina
comedy.
Miss Lake zone
Intercolleges 2012 inayoandaliwa na kampuni ya Angles Real Entertainment ya
jijini Dar es salaam chini ya Mkurugezi wake Joseph Rwebangira imejipanga vya
kutosha kuleta mabadiliko ikiwa na lengo la kumfikisha mrembo wake katika ngazi
ya fainali kitaifa.
Shindano hilo
litafanyika katika ukumbi wa Linuz Club uliopo Bukoba mjini siku ya jumamosi
tarehe 23 juni ambapo mbali ya hayo
kutakuwa na burudani za ngoma za asili na wasanii wa mkoa wa Kagera,pia
kiingilio kitakuwa ni Tsh 10,000/= kawaida na V.I.P ni Tshs 15,000/=