Mrembo atakayeiwakilisha
Nchi ya Malawi katika mashindano ya Miss East Africa
2012 ametangazwa rasmi baada ya kuwashinda wenzake 39 waliojitokeza kutaka
kuiwakilisha Malawi katika mashindano hayo.
Mrembo huyo ni Miss
Elidas Ella Chirwa (22) mwenye urefu wa 1.82m ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu
katika Chuo kikuu cha Malawi.
Fainali za mashindano ya
Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 September mwaka huu jijini Dar es
salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,
Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion,
Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East
Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar
es salaam