MKuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Saidq akikabidhi bendera
RAIS Jakaya
Mrisho Kikwete amewapongeza wachezaji wa timu ya soka ya Tanzania ,
Kili Taifa Stars
kuimarika kimchezo hadi kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia
katika mechi ya
Jumapili iliyopita kwenye kampeni ya kucheza fainali za Kombe la Dunia
za mwaka 2014.
Pongezi hizo zilifikishwa
kwa wachezaji wa timu hiyo leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,
Said Meck Sadiq
wakati wa hafla ya kuiaga kwenye hoteli ya Tansoma, kabla ya kuondoka
leo kwenda
Msumbiji kwa mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Afrika zitakazopigwa mwakani
nchini Afrika
Kusini.
Akimnukuu
Rais Kikwete, Sadiq alisema, ushindi huo wa Jumapili, umeleta heshima
na
kuonesha kuwa wanaweza kama watadhamiria,
hivyo waongeze juhudi katika kupigania mafanikio ya timu hiyo katika michuano
ya kimataifa.
Stars
iliyoagwa jana, inaondoka leo asubuhi kwenda Msumbiji kwa mechi ya
Marudiano
itakayochezwa kwesho kwenye Uwanja wa Taifa uliopo katika eneo la Zampeto, nje
kidogo ya Jiji la Maputo
kuanzia saa 9 mchana kwa saa za huko.
Alisema,ushindi
huo umekuwa faraja kwa wapenzi na mashabiki wa soka nchini
ambao
hujitokeza uwanjani kuishangilia na kuwasihi waendelee kutimiza wajibu
wao
kwa timu hiyo iliyo chini ya Kocha Kim
Poulsen.
Amewataka
wachezaji hao kuzingatia mafunzo ya makocha wao na kuongeza ya kwao huku
wakidumisha nidhamu ya ndani na nje ya uwanja ili kupata ushindi katika michezo
mbalimbali.
“Nina
uhakika mmeandaliwa vizuri, tena kwa kiwango kinachostahili, hivyo ari mliyoonyesha
kipindi hiki, iendelee, isionekane kama mmebahatisha…si
kwa
Msumbiji
tu, bali kwa timu yoyote mtakayokutana nayo,”alisema.
Awali,
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodger Tenga aliwasihi nyota hao kuiwakilisha
vema Tanzania
katika mechi hiyo, wakijituma wakizingatia
mafunzo
na
maelekezo ya makocha wao kupata ushindi kwani watanzania wanawategemea.
“Mnakwenda
kwenye mechi muhimu sana , tuna imani mtafanya
vema kulingana na kiwango kizuri mlichionyesha Jumapili mlipocheza na Gambia ,
hivyo nina uhakika mtarejea na ushindi na niwatakieni kila la heri,”alisema
Tenga.
Naye
Poulsen alisema, amekiandaa vema kikosi chake, akinimini watayatumia vema
mafunzo aliyowapa kushinda mechi hiyo ambayo anaamini itakuwa ngumu na yenye
ushindani mkubwa.
Alisema,
kwa kipindi alichokaa na wachezaji, anafurahi kuona viwango vyao, vimekuwa
vikiimarika kila siku, ingawa kuna baadhi ya idara na hasa safu ya ushambuliaji, imekuwa na udhaifu ambayo
inahitaji kazi ya ziada.
“Tunakwenda
na akili za kushinda ili kupata mafanikio mazuri huko tuendapo katika mchakato
huu wa kusaka tiketi, hivyo ninamatumaini wachezaji watatumia vema mafunzoi
yangu na kushinda mchezo huo,”alisema Kim.
Aidha,
msafara wa timu hiyo utakaohusisha wachezaji 20 utaondoka bila ya nyota wake
watatu ambao ni majeruhi, akiwemo kipa
Mwadini Ali na mabeki Nassoro Masoud Cholo na Waziri Salum.
Kama
Stars itaing’oa Msumbiji, katika raundi
ya mwisho itapangiwa moja kati ya timu 16 zilizocheza Fainali za AFCON zilizopita
nchini Gabon na Equatorial Guinea ambako Zambia
walitwaa ubingwa kwa kuwafunga Ivory
Coast .
Katika
mechi yao ya kwanza iliyopigwa Februari 29,
kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ,
timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, hivyo Stars itapaswa kupata ushindi katika
mechi ya kesho kama inataka kusonga mbele.