Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Sothern Sudan katika
mashindano ya Miss East Africa 2012 amepatikana.
Mrembo huyo ni Miss
Akuot Philip Suzan (20) mwenye urefu
wa futi 6.1 anaekaa Juba, Sudan ni
mwanamitindo Nchini humo na anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha makelele
Nchini Uganda mwaka huu.
Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika Nchi
mbalimbali kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritrea: Miss
Rahwa Afeworki (22), kutoka Ethiopia
ni: Miss Lula Teklehaimanot (19) na Miss Ayisha Nagudi (23) ambae ni
mwakilishi wa Uganda.
Nchi zilizobaki zinaendelea kutafuta wawakilishi
watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ambayo
yatazishirikisha Nchi 16 za ukanda huu ambazo ni Tanzania (wenyeji), Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine ni Southern Sudan, Somalia, Djibouti,
Eritrea, Ethiopia pamoja na visiwa vya Mauritius, Madagascar, Comoros, Reunion
na Seychelles.
Mashindano ya Miss East Africa ndio mashindano makubwa ya
urembo kwa ukanda huu wa Africa.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa ambazo huandaliwa
na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events
Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam, Tanzania.