RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Leoder Tenga amesema hakubaliana na suala la nyota wa timu hiyo Kelvin
Yondan kusaini mikataba miwili na kusema kuwa lazima kuna moja ya klabu
imefanya uhuni katika mchakato huo.
Tenga
alisema kuwa, kulingana na mfumo wa sasa wa usajili kupitia mtandao, shirikisho
lake halihusiki
kabisa na usajili na kwamba hilo
ni suala la mchezaji na klabu.
“Naamini
klabu hizo zitamalizana zenyewe kuhusu mchezaji huyo na akasema suala la Yondan
kudaiwa kutoroshwa kambini, Taifa Stars ili akasaini Yanga halina mantiki kwa
sababu mchezaji huyo ni mtu mzima ana akili zake timamu, ila kinachoendelea kwa
sasa ni kelele za kinazi,”alisema
Wiki
iliyopita, beki Yondan aliibuka anasaini Yanga, kabla ya klabu yake, Simba
aliyoichezea tangu mwaka 2006 kudai bado ina mkataba naye na wapinzani wao hao
wa jadi, wamefanya uhuni kuzungumza naye na kumsajili wakijua hajamaliza
mkataba na klabu yake.
Lakini
Yondan mwenyewe alikana kusaini Simba na kusistiza amesaini Yanga tu, waliompa
Sh. Milioni 30 kwa mkataba wa miaka miwili.