MGOMBEA huyu anasema amejitosa kuwania nafasi hiyo ili kuweza
kusaidia kutatua matatizo mengi yanayoikabili klabu ya Yanga ikiwemo mishahara
ya wachezaji na kocha.
Tindwa
alisema hayo yatatimia iwapo wanachama wa Yanga watampa ridhaa ya kuongoza
klabu hiyo.
“Kama
nitachagulia nitasimama kidete kuhakikisha makocha na wachezaji wanalipwa
mishahara kwa wakati kwani bila wao kulipwa ama kuhudumiwa vizuri hakuna mafanikio
yoyote na ndio chanzo cha migogoro,”anasema .
“Mimi si ni mwanachama tu wa
Yanga bali ni mwanamichezo mwenye uchu wa maendeleo, hivyo nitasimama kidete
kuisaidia Yanga kujitegemea yenyewe,”anaongeza.
Mbali na hilo ,
Tindwa amepania kusaidia kutafuta wachezaji mahiri watakaoitumikia klabu hiyo kama alivyofanya kwa Gula Joshua na wengine.
“Napenda kuwasikhi wanachama
wenzangu kwa kuchagua viongozi wenye kuisaidia timu yetu na si kutaka
kujinufaisha,”alisema.