Francis Kaswahili
Kamati ya uchaguzi ya klabu
hiyo imetoa hadhari juu ya uwepo wa kampeni chafu.
Katibu wa kamati ya uchaguzi
ya Yanga Francis Kaswahili amesema kwamba kuna baadhi ya wanachama
wamekuwa wakipitisha karatasi yenye nembo ya Yanga ikiwatambuylisha baadhi ya
wagombea kuwa ndio wameteuliwa kuongoza klabu hiyo.
Alisema kufanya hivyo ni
kuingilia misingi na haki za wagombea wengine hivyo watakaobainika atachukuliwa
hatua kali za kinidhamu na kuongeza kuwa Kamati ya uchaguzi ya Yanga ndiyo ina
mamlaka ya kumtangaza mshindi.
Aidha, Kaswahili alitoa onyo
kwa baadhi ya wanachama kutishia kwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi na
kusema kuwa atakayefanya hivyo atashitakiwa kwa kamati ya nidhamu ya Yanga
kabla ya kufutwa uanachama.