Timu ya Taifa ya Rwanda ya vijana wenye umri chini
ya miaka 20 inatarajia kuwasili Dar es Salaam leo mchana (Julai 13 mwaka huu)
kwa ndege ya RwandAir kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ngorongoro
Heroes.
Ngorongoro Heroes tayari iko kambini chini ya Kocha Jakob
Michelsen na msaidizi wake Adolf Rishard kujiwinda kwa mechi hizo ambazo ni
sehemu ya maandalizi ya kuivaa Nigeria .
Mechi dhidi ya Nigeria
ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili kusaka tiketi ya kucheza fainali za
Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Algeria
itachezwa Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .