MICHUANO ya Kombe la Mwakalebela, inatarajiwa kuanza kutimua
vumbi mjini Iringa, kuanzia Julai saba, huku ikishirikisha michezo ya
Netiboli na mpira wa Miguu kwa timu za
Iringa mjini.
Michuano hiyo ni muendelezo wa kuendeleza michezo kwa mdau
wa michezo, Fredrick Mwakalebela (pichani), aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Soka nchini (TFF).
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam , Mwakalebela, alisema kwamba
kwa netiboli, timu za kwenye kata 16 zitashiriki.
Alisema kwamba anaamini kwa kuanzisha michuano
hiyo,mambo yatakuwa mazuri na kuwafanya
wanamichezo kujiweka katika ramani nzuri kimichezo.
Lengo langu ni kufanya wanamichezo wajiweke katika kiwango
cha juu,hivyo naamini huu ni wakati wao vijana kufanya kazi ya maana.
Naamini kila siku kinachotakiwa kufanywa ni kuwekeza katika
michezo, hivyo lengo halisi litajulikana na kuendeleza michezo mkoani Iringa na
Tanzania
kwa ujumla,” alisema Mwakalebela.
Kata ambazo zitachuana kwa timu za wanawake za netiboli ni
pamoja na Ruaha, Kigonzila, Mshindo, Mwangata, Gongilonga na nyinginezo
zinazounda jimbo la Iringa Mjini.
Aidha katika timu zinazotarajiwa kushiriki katika michuano
hiyo ya Mwakalebela Cup ni pamoja na Lipuli, African Wonders na nyinginezo
zilizosheheni wanamichezo wenye uwezo wa juu.
Mwakalebela ni miongoni mwa wadau makini w2a mpira wa
miguu,huku akikumbukwa na wengi kwa utendaji kazi wake mzuri na uliochangia kwa
kiasi kikubwa kukuza mpira wa miguu.
Baada ya kumaliza kipindi cha uongozi wa TFF, Mwakalebela,
alikwenda kuwania ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, hata hivyo
alienguliwa na chama chake.