Tanzania
imependa kwa nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya ubora ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Julai 4 mwaka huu) na
shirikisho hilo.
Kwa viwango vya Juni mwaka huu, Tanzania (Taifa Stars) ambayo timu
yake inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 139 hivi sasa
imefika nafasi ya 127 ikiwa na pointi 253 kulinganisha na 214 za Juni mwaka
huu.
Ivory
Coast inayoshika nafasi ya 16 duniani bado
inaongoza kwa upande wa Afrika ikiwa na pointi 939. Timu hiyo ilikuwa katika
nafasi hiyo hiyo kwa viwango vilivyotolewa Juni 6 mwaka huu. Hispania ambao ni
mabingwa wa Ulaya na Dunia ndiyo wanaoendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya
kwanza wakiwa na pointi 1,691.