Timu 10 za Tanzania Bara zitashiriki kwenye michuano ya
Rollingstone kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 ambayo mwaka huu
itafanyika Makamba nchini Burundi
kuanzia Julai 7 mwaka huu.
Jumla ya timu 24 zinashiriki mashindano hayo na zimepangwa
katika makundi sita tofauti. Timu nyingine zinatoka Burundi ,
Kenya , Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC), Uganda
na Zanzibar .
Timu za Tanzania zilizoingia katika mashindano hayo ni Azam,
Bishop High School, Chakyi Academy, Coastal Union, Rollingstone, Ruvu Shooting,
Simba, TAYFA Academy, Yanga na Young Life.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Rollingstone, Issa Karata timu
zote zinatakiwa kwenda vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji wake ili kuthibitisha
umri wao. Kamati ya Mashindano itakuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu umri wa
mchezaji yeyote.
Kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji 20 na viongozi watano
ambao watagharamiwa na waandaaji kwa huduma za malazi na chakula kwa muda wote
wa mashindano hayo yaliyoanzishwa miaka 13 iliyopita.