WAKATI kampeni kwa wanaowania
uongozi katika klabu ya soka ya Yanga zikitarajiwa kuanza ijumaa, kamati ya
uchaguzi ya klabu hiyo imewataka baadhi ya wagombea kuwasilisha nakala halisi
ya vyeti vyao vya sekondari.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Yanga, Jaji mstaafu John
Mkwawa alisema kwamba mwisho wa kuwasilisha vyeti hivyo ni kesho na baada ya hapo
ndipo wataendelea na taratibu nyingine za uchaguzi.
Jaji Mkwawa aliwataja
wagombea hao ni pamoja na Sarah Ramadhan anayewania nafasi ya uenyekiti,
Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti, Edger Fongo, Ramadhan Kampira, Mohammed
Mbaraka, Abdallah Binkleb na Omary Ndula.
“Kamati inawaagiza wagombea
hawa kuwakilisha nakala zao halisi za vyeti vya sokendari mpaka kufikia kesho
(leo), hivyo kamati inasisitiza hilo
ili tuweze kuendelea na hatua zinazofuata,”alisema.
Uchaguzi mdogo wa viongozi wa
Yanga unatarajiwa kufanyika Julai 15 mwaka huu katika ukumbi utakaotangazwa
baadaye ambapo nafasi za mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wanne wa
kamati ya utendaji zitajazwa.
Wagombea waliokidhi vigezo
mpaka sasa ni pamoja na Jonh Paul Jambele, Yusuf Manji na Edgar W. Chibula
wanaowania Uenyekiti, Ayoub Nyenze na Yono Stanley Kevela.wanaowania nafasi ya
makamu mwenyekiti, huku Jumanne Mwamenywa, Beda Tindwa,Ramadhan Said,Shaban
Katwila na Lameck Nyambaya wakiwania ujumbe.
Wengine ni Peter H. Haule, Justine S. Baruti Yono Kevela, Mosess K.
Valentino, Aaron Nyanda, George M. Manyama,Abdalah Sharia Ameir,Jamal Kisongo na Gaudiusus Ishengoma ambao pia
wanawania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.