Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela akizungumza na Mashabiki, Wadau na Wananchi wa Rungwe wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kuifufua timu ya Tukuyu Star kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu mkoani Mbeya leo, ambapo kulikuwa na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu ikishereheswa na ngoma za asili ya watu wa Rungwe ya Ighoma iliyokuwa ikutumbuizwa katika viwanja hivyo, Bonanza lilivuta hisia za watu wengi na wadau wa mkoa wa mbeya na mikoa ya jirani hasa wachezaji waliowahi kuchezea timu ya Tukuyu Star miaka ya 1980 na 1986 huku umati wa watu ukishuhudia tukio hilo. Katika bonanza hilo timu ya Rungwe Veterani imefaikiwa kkuichapa timu ya wadau wa Tukuyu Star Family magolo 3-1, akielezea mpambano huo Kocha wa timu ya Tukuyu Star Family Kenny6 Mwaisabula amesema kushindwa ni sehemu ya mchezo, lakini pia wachezaji wa Rungwe Veterani wako fiti zaidi kimchezo kutokana na kwamba muda mwingi wanafanya mazoezi sana, lakini pia hali ya hewa inawaruhusu kwani wamezoea baridi tofauti na wachezaji wake, Usiku huu kuna kongamano linaendelea mjini Tukuyu ili kujadili mikakati mbalimbali na utaratibu utakaotumika katika kuiendesha Tukuyu Star mpya. |
|
|