MAKAMISHNA, WAAMUZI WA DARAJA LA KWANZA KUNOLEWA


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina kwa ajili ya makamishna (match commissioners), watathmini wa waamuzi (referees assessors) na waamuzi wa daraja la kwanza (class one) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ligi Kuu inayotarajia kuanza baadaye mwezi ujao. 
Kwa upande wa makamishna na watathmini wa waamuzi, semina itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 29-30 mwaka huu. Washiriki wanatakiwa kujigharamia kwa kila kitu; usafiri, malazi na chakula wawapo kwenye semina. 
Semina kwa waamuzi itafanyika katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza kuanzia Agosti 31- Septemba 2 mwaka huu. Pia nao watajigharamia kwa kila tu. Waamuzi watakaoshiriki semina hiyo ni ambao hawakushiriki ile iliyofanyika Juni mwaka huu na wale walioshiriki lakini hawakufaulu mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test).

Waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) hawashiriki kwa vile wao wamekukuwa wakishiriki semina zao zinazoandaliwa na FIFA kila baada ya miezi mitatu.

Post a Comment

Previous Post Next Post