Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime
KOCHA wa timu ya Mtibwa
Sugar,Merky Mexime,amesema wachezaji wakimataifahawana nafasi katika kikosi
chake.
Mexime alisema wachezaji wengi wa kigeni
wanaokuja nchini hawana uwezo uanjani licha ya kukumbatiwa na klabu kubwa.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa,Taifa
Star”,alisema wachezaji wazalendo wanamchango mkubwa katika klabu za soka.
Alisema Tanzania ina
wachezaji wazuri na wana uwezo mzuri,lakini hawapewi nafasi kima ilivyo wakimataifa
wanaogeuka lulu.
“Natamani hata wasije kucheza
nchini,hawana lolote kulinganisha na wachezaji wetu ndio maana mtibwa
hatusajili wachezaji wa kigeni.”alisema Mexime.
Alisema klabu za Simba na
Yanga zinapaswa kubadilika na kuwatumia wachezaji wazalendo ili kuongeza
viwango vyao vya soka.
Alisema wachezaji wa Tanzania
wakitumika vyema wana nafasi kubwa ya kupata timu nje ya nchi.
Mbali na Simba na Yanga,Azam ambayo imekuwa tishio kwa vigogo
hivyo ni miongoni mwa klabu zilizosajili wachezaji wa kimataifa .
Yanga ina kipa yam
Berko,Hamisi Kiiza na Haruna Niyonzima.
Simba ni Emmanuel Okwi,Felex Suzu na Azam ni
Kipre Tchetche.
CHANZO:Gazeti la Uhuru