MSONDO NGOMA
SIKINDE NGOMA YA UKAE
Na Mwandishi Wetu
Bendi zenye upinzani wa jadi nchini kama
ule wa Simba na Yanga, Msondo Ngoma Music Band na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya
Ukae) zitapambana siku ya Iddi Mosi
kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni.
Tayari mashabiki wa bendi hizo wameanza maandalizi ya
kuzishangilia bendi zao.
Mpambano
huo umeandaliwa na kampuni za Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.
Mratibu wa
mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu
ya Iddi na kuamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa
dansi nchini kwa mwaka 2012.
Kapinga
alisema ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa, kila bendi itatumia jukwaa lake kwa
kupiga kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani.
“Litakuwa
pamabano la aina yake ukizingatia kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa bendi hizi
pinzani kupambana siku ya sikukuu ya Iddi tangu zianzishwe” alisema Kapinga.
“Pia
itakuwa ni mara ya kwanza kwao kushindana katika viwanja vya Leaders Club.”
Kapinga
alisema kampuni yake inafanya mipango ya kuwasafirisha wapenzi wa bendi hizo
kutoka kila wilaya ya Dar es Salaam kuja kushuhudia mpambano huo.
Alisema
mchuano huo itaanza saa nane mchana hadi liamba.
Mwaka jana
bendi hizo zilipambana vikali kwenye ukumbi wa TCC Club sikukuu ya Krismasi
ambapo mbali na muziki safi na vituko vya hapa na pale kama ilivyo kawaida,
zilitoka sare kwa kupata pointi sawa.
Mratibu
amesema kuwa mwaka huu mshindi ni lazima apatikane hata kwa kurusha shilingi.