Meneja masoko wa kampuni ya G-Tide inayozalisha simu za mkononi aina ya G-Tide Mbwana Mtopa kushoto , pamoja na ofisa wa kampuni hiyo Chile Kasoga na Meneja wa G-Tide Nemes Kilegulo wakionesha wanahabari simu mpya ambazo unaweza kuunganishwa na huduma ya Easy Talk.
KAMPUNI inayozalisha simu za mkononi aina ya G-Tide imehamasisha wananchi kununua simu
zinazozalishwa na kampuni hiyo ili kujiunga na huduma mpya ya mawasiliano ya
ujumbe wa sauti ijulikanayo kama Easy
Talk.
Meneja Masoko wa kampuni hiyo Mbwana Mtopa alisema kwamba huduma
hiyo ni nzuri na ya gharama nafuu ambayo inawawezesha watumiaji kuwasiliana
pamoja kwa njia mbalimbali.
Alisema kupitia huduma hiyo
mteja wa mtandao wowote wa simu za mkononi nchini ambaye anatumia simu za
G-Tide akijiunga na mtandao wa Intanet anaweza kuwasiliana na watumiaji wengine
wa simu hizo kwa gharama za chini zaidi.
Mtopa alisema mbali na ujumbe
wa sauti, Easy Talk pia inahusisha kupunguza gharama ya kupiga simu kwa kuchat
na watu pamoja na makundi tofauti.
“Mfano umenunua intaneti
katika mtandao fulani wa simu kwa MB 40 tu unaweza kutumia huduma zote za Easy Talk kwa mwezi mzima,”alisema