Kocha wa Stars, Kim Poulsen
Na Mwandishi Maalumu, Gaborone ,
Botswana
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen
ameanza kazi ya kutengeza washambuliaji wapya katika kikosi chake huku akianza
na Haruna Moshi ‘Boban’.
Kocha huyo ameamuwa kutengeneza safu ya washambuliaji ili
timu hiyo iweze kuwa na hazina ya washambuliaji wenye uchu wa kupachika mabao.
Stars ambayo inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium
Lager inajiandaa kucheza mechi za kuwania kufuzi nafasi ya kucheza fainali za
Kombe la Dunia nchini Brazil
mwaka 2018.
Akizungumza na Boban jana (juzi) usiku baada ya mazoezi ya
timu hiyo hapa mjini Gaborone nchini
Botswana Poulsen alisema “Wewe ni
mchezaji mzuri sana na una uwezo mkubwa wa kuisaidia timu, na kuanzia leo
ninakupa jukumu la kucheza kama mshambuliaji na si kiungo mshambuliaji”alisema
Poulsen na kuongeza:
“Nakupa kazi hii kwa sababu nimegundua kuwa ukicheza kama
mshambuliaji unaweza kufunga magoli mengi kuliko ukicheza kama
kiungo, sababu ya msingi ni kwamba ninataka uzibe pengo lililoanza kujitokeza
hivi sasa, baada ya Mbwana Samatta,Thomas Ulimwengu,na John Bocco kukosekana”.
Katika mazungumzo ya kocha huyo yaliyodumu kwa zaidi ya
dakika 15 baada ya mazoezi, Poulsen aliendelea kumwambia Boban kwamba, “katika
kikosi changu wewe ndiyo mchezaji mwenye uzoefu mkubwa kuliko wote na
nimegundua kwamba hata wachezaji pia wanakuheshimu na mnashirikiana vizuri,
ndani na nje ya uwanja mbali na hilo wewe ni kati ya wachezaji wanaotambua
wajibu wao ndani na nje ya Uwanja,sawa Moshi”.
Baada ya Poulsen kuzungumza na Boban alisema kwamba kuanzia
sasa Boban atakuwa akicheza kama mshambuliaji katika timu hiyo na si kama kiungo mshambuliaji.
Alisema Boban ni mchezaji mwenye akili sana na asiye na papara anapokuwa ndani ya
eneo la kufunga na kwamba ni kati wachezaji wachache wanaocheza nafasi ya
kiungo wenye uwezo wa kufunga.
Akielezea sifa za Boban Poulsen alisema kwanza sifa ya
mshambuliaji mzuri ni yule asiyekuwa na ubinafsi kwamba lazima afunge yeye,na
Boban ana sifa hiyo, Boban sio mchoyo wa kutoa pasi anapoona kwamba hawezi
kuendelea kukaa na mpira wakati kuna mtu mwingine ana nafasi lazima atoe pasi.
“Ukiwa na mchezaji kama huyu pale mbele nilazima upate
ushindi kwa sababu mabeki watakuwa akimlinda sana
yeye wakijua kwamba atafunga yeye kumbe anatoa pasi kwa mfungaji mwingine, na hilo ndiyo tatizo la
wachezaji watanzania, kwani hawachezi kitimu mshambuliaji anajuwa kuwa yeye
ndiyo mwenye jukumu la kufunga peke yake kumbe sivyo”.
Akizungumza vitu vichache ambavyo anapaswa kumpatia Boban
ili aweze kumudu nafasi hiyo vizuri Poulsen alisema kuwa ni pamoja na
kujitambua kuwa yeye sasa ni mshambuliaji na si kiungo, kuongeza uwezo wa
kujiamini kwamba anaweza kukabiliana na beki wa aina yeyote,kuongeza kasi na
kufanya maamuzi ya haraka, na kuwahamasisha wenzake kuwa kila kitu kinawezekana
hasa pale anapofanikiwa kufunga goli.
Katika hatua nyingine alisema kwamba timu iko vizuri na
hakuna majeruhi hata moja na kwamba hana
wasiwasi wowote juu ya mechi hiyo.
Kwa upande wake Boban alisema kwamba amekubaliana na uwamuzi
wa Mwalimu kwa sababu amegundua kwamba akicheza kama mshambuliaji ataisaidia
timu zaidi kuliko akicheza kama kiungo hivyo yeye kama
mchezaji hana tatizo na atafuata ushauri wa mwalimu.
“Mimi sina tatizo kwakuwa Kocha mwenyewe ndo ameona hivyo
basi mimi sioni ugumu wowote kwa sababu najua kufunga na lengo ni kuisaidia
timu yetu ipate ushindi.
Matokeo??????????
ReplyDelete