NUSU fainali ya michuano ya
BancABC SUP8R inatarajiwa kutimua vumbi leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa mechi mbili kupigwa kwenye dimba hilo .
Simba watashuka dimbanikuwakabili Wanalambalamba Azam FC huku mechi ya kwanza ikichezwa mapema
kuanzia saa 8:00 kati ya Jamhuri ya Pemba na
Mtibwa Sugar.
Ofisa habari wa Simba alisema wamejipanga vya kutosha na ana imani vijana wake watapigana kufa
au kupona ili kulileta kombe hilo
Msimbazi, maana ni kama kawaida yao michuano yoyote inapoanza, kubeba ubingwa. "Hii BancABC SUP8R, ni ya
kwanza, kwa hiyo kombe ni la Msimbazi japokuwa lolote linaweza tokea,” alisema
Kamwaga.
Naye Kocha Mkuu wa Jamhuri, Amiry
Chuwa, alisema wao leo watapambana kuhakikisha wanashinda ili kutinga fainali,
kutokana na maandalizi waliyofanya tangu kuanza kwa michuano hiyo.
Naye Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky
Mexime, alisema wanajiamini katika
mchezo huo kutokana na kiwango chao huku akiwataka wadhamini BancABC SUP8R,
kutokata tamaa kwa kuwa soka la bongo lina zengwe.
“Soka la bongo ni zengwe tupu,
hivyo nyie wadhamini nawashauri msikate tamaa, muhimu muwe na mioyo migumu
msitishwe na zengwe, mkifanya hivyo mtapata tabu sana , ” aliwashauri Mexime.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
BancABC, Boniface Nyoni, amesema wao kama wadhamini, wataendelea kufanya kazi
zao kwa ushirikiano mkubwa na vyombo vya
habari na Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF).
Michuano hii ambayo ilishirikisha
timu nane za Simba, Azam FC, Mtibwa, Polisi Morogoro, Super Falcon, Mtende,
Zimamoto na Jamhuri, inatarajiwa kufikia tamati Jumamosi.
Bingwa wa michuano hiyo,
atajinyakulia kitita cha sh mil. 40; wa pili sh mil. 20 na waliotinga nusu
fainali kila mmoja sh mil. 15 na waliosalia sh mil 5 kila mmoja