KUTOKANA na shirikisho la soka Tanzania (TFF) kusogeza
mbele tarehe ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara, Simba itaendelea kujichimbia Arusha hadi
Septemba 6 itakaporejea jijini Dar es Salam kwa ajili ya mechi yake ya kuwania
ngao ya jamii dhidi ya Azam Fc itakayopigwa Septemba 8.
Awali Simba na Azam zilikuwa zicheze mechi hiyo Agosti 25 na
kutokana na mabadiliko hayo wameliagiza benchi la ufundi la klabu hiyo kukutana
ili kupanga program.