Msanii wa Filamu Nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto akizungumza na waandishi wa habari wakati walipokuwa wanatoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuwa wameungana kupambana na maalamia wa kazi zao za sanaa kushoto ni
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na msanii Muhsin Hawadh.
Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB' kushoto akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo juu ya wizi mkubwa uliotokea hivi karibuni uliofanywa na Kampuni ya Steps Entatainment kwa kushirikiana na wasanii wwenyewe na kudai kuwa tabia hii ikomeshwa kwa maalamia wa kazi za wasanii kulia ni Msanii Vicent Kigos 'Ray' na Mwenyekiti wa Shilikisho la Filamu Tanzania 'TAFF' sIMON mWakifwamba
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama katikati akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam baada ya wasambazaji kuungana na wasanii kwa ajili ya kutoa tamko la kupambana na malamia wa kazi za sanaa kushoto ni msanii Muhsin Hawadhi na Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB' (Picha zote na www.burudan.blogspot.com)
SHIRIKISHO la Filamu
nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni
za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘zimeapa’ kupambana na maharamia
wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya wasanii.
Wakizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema
umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili
kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba,
mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya
kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe
ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa Serikali
kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa
maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa
watu wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza
kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa
hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika
nayo” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi
Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia
pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja
na utalii.
Alisema Serikali inapswa
kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili
kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya
kazi zao.
Kwa upande wake Meneja
usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti
wizi wa kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge
lake kukubalina kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.
Ambapo wasanii na wasambazaji
wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwebnda kwa
haki ili wasanii wapate na wao wawe ni watu wa kusaidi wasanii kusambaza kazi
zao