SIKU chache
baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama
Kombe la Kagame klabu ya soka ya Azam Fc imemtimua kocha wake mkuu Muingereza
Stewart Halll, imefahamika.
Habari
kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kwamba sababu ya kumtimua kocha huyo ni
kitendo cha kumpanga nyota wa timu hiyo Mrisho Ngassa katika mechi ya fainali
ya Kombe la Kagame baina ya Azam na Yanga ambapo Yanga ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Azam mabao 2-0.
Inaelezwa
kuwa uongozi ulikerwa na kitendo cha Ngassa ambaye kwa muda mrefu amekuwa
akituhumiwa kuwa na ‘Uyanga’ na hivyo kocha kumuweka benchi katika mechi za
kombe la Kagame, alipoibusu na kuvaa jezi ya Yanga baada ya mchezo baina ya
Azam na Vita.
Ukishinda hata kwa kubahatisha kochwa anafaa, ukishindwa kocha hata ni mzuri vipi hana lake, hafai!
ReplyDelete