ZIARA
ya timu AFC Leopards ya Kenya iliyokuwa
itue nchini imeota mbawa.
Leopards
inayoshiri Ligi kuu ya Kenya
ilikuwa icheze na vigogo vya soka nchini Simba na Yanga ambapo leo ilitarajiwa
kucheza na Simba katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Mmoja ya waratibu wa ziara hiyo George Wakuganda
alisema wameamua kufuta ziara hiyo kutokana na kukosekana kwa viwanja.
Alisema
wamiliki wa uwanja wa Sheikh Amri Abeid wameshindwa kuruhusu kutumika uwanja
huo kwa ajili ya mechi kutokana na kuwa katika matengenezo.
Aliongeza
kuwa, hata mchezo baina ya Leopard na Yanga ambao ulipangwa kuchezwa Jumanne
ijayo kwenye Uwanja wa taifa
Dar es Salaam nao hautakuwepo kwa sababu ya kukosekana kwa uwanja.