Wanamichezo 15 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA)
utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
Waliochukua fomu za kuwania uenyekiti ni Lina Kessy,
Isabellah Kapera na Joan Minja. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeombwa na
Roseleen Kisiwa pekee wakati Katibu Mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Makafu.
Macky Mhango pia ni mwombaji pekee aliyeomba nafasi ya Katibu Msaidizi.
Waombaji watatu wa nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Furaha Francis, Juliet Mndeme na
Zena Chande. Nafasi ya Mhazini nayo ina mwombaji mmoja tu ambaye ni Rose
Msamila.
Sophia Charles, Rahim Maguza, Telephonia Temba na Jasmin
Badar Soud wao wanaomba nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho
kwenye uchaguzi huo ambao utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya
Ombeni Zavalla.