Klabu za Ligi Kuu na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu
za mkononi ya Vodacom zimekutana jana (Septemba 27 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
Mazungumzo yalilenga kipengele ya upekee (exclusivity)
kilichopo kwenye mkataba wa udhamini ambacho kitaendelea kuwepo. Klabu zilikuwa
zimeomba kwa mdhamini kuangalia uwezekano wa kukiondoa.
Pande hizo zimekubaliana kuunda kamati ya pamoja kwa ajili
ya kuitafutia kila klabu mdhamini binafsi kwa lengo la kuhakikisha zinashiriki
kikamilifu katika ligi hiyo.
Klabu zote zimeshapata vifaa kutoka kwa Vodacom ukiondoa
African Lyon ambayo ilitarajia kuchukua vifaa hivyo leo kutoka kwa mdhamini wa
ligi hiyo.