Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom,Rene Meza akimfafanulia jinsi mkataba ulivyo wa udhamini wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ,Said Mohamee,katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam,wanaoshuhudia wapili toka kushoto Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani,Ofisa Mkuu wa maswala ya Sheria wa Vodacom Bw.Wallarick Nittu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom,Rene Meza akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi , Mohammed Said mkataba wa udhimini wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara,katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kampuni
ya Vodacom imekuwa mdhamini wa ligi kuu kwa miaka mitano iliyopita, na sasa
imeingia mkataba mpya wa udhamini kwa miaka mitatu na TFF, mkataba utakao
liwezesha shirikisho hilo
kupoea fedha za udhamini kwa miaka mitatu.
Ligi
kuu ya Vodacom itaanza tarehe 15 ya mwezi huu, ikitarajia kushuhudia michezo
182 ikichezwa katika viwanja mbalimbali na kushirikisha timu 14, zikiwemo timu
za Dar es Salaam Young Africans, Kagera Sugar na Simba Sports Club ambaye
ndie bingwa mtetetzi wa kombe hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania , Rene Meza, amesema kuwa
kampuni ya Vodacom iko katika mstari wa mbele katika kuunga mkono maendeleo na
shughuli mbalimbali za kimichezo ndani ya nchi.
“Wanamichezo wote ni mabalozi wazuri katika nchi. Ni wajibu wetu
kuhakikisha kuwa tunawaunga mkono katika kutambua na kukuza vipaji vyao kadri
tutakavyo weza,” alisema Meza na kuongeza kuwa, “Kama jina linavyojulikana ligi
kuu ya Vodacom, kombe hili linashuhudiwa na mashabiki zaidi ya milioni 10
katika mechi 182 zitakazo chezwa sehemu mbalimbali za Tanzania bara.”
Meza amejivunia
kampuni hiyo kuwa wadhmini wa ligi kuu kwa kipindi kingine, na kufafanua kuwa
mpira wa miguu ndio unaongoza kitaifa na unapendwa na Watanzania wengi.
Michuano ya mwaka huu itashuhudia timu mpya tatu ambazo ni timu ya Polisi Morogoro , Tanzania Prisons na Mgambo JKT.
Mkataba huu umehusisha pande zote ambazo ni kampuni ya Vodacom Tanzania ,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kamati ya ligi.
Kwa upande wake makamu wa Rais wa TFF, Nasibu Nyamlani, ameipongeza
kampuni ya Vodacom Tanzania
akisema kuwa anaamini kuwa maendeleo ya sasa yatalenga zaidi katika kuunga
mkono vipaji vipya na vilivyopo ndani ya nchi.
“Kwa niaba ya TFF, napenda kuwashukuru Vodacom Tanzania kwa
kuonyesha nia na kuendelea kuunga mkono mpira wa miguu nchini. Nasi tunaahidi
kuendelea kuthamini vipaji vya wachezaji wetu na kuhakikisha tunapata mafanikio
zaidi,” alisema Nyamlani.