KATIBU
Mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi amefanikiwa kukata
tiketi ya kushiriki mkutano mkuu wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
akiwakilisha Wilaya ya Karatu.
Bayi
amefanikiwa kukata tiketi hiyo kupitia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni baada
ya kupata kura 264, ambapo ataungana na Mary Sulley(545), Ori Pembe (460),
Fabiola Deo (456) na Amsi aliyepata kura 322.
Katika
uchaguzi huo, nafasi ya uenyekiti ilikwenda kwa Mustafa Mbwambo aliyepata kura
512 na hivyo kumwangusha Gerald Gwaha
aliyepata kura 148 huku mgombea mwingine
aliyefahamika kwa jina la Tippe alijitoa katika kinyang’anyiro hicho.
Kwa
upande wa nafasi kamati kuu ya halmashauri kuu (NEC)Awaki Tlemai alishika
nafasi ya kwanza kwa kupata kura 545 na Daniel Ilakwahhi aliyekuwa wa pili kwa
kupata kura 114.