UONGOZI
wa Klabu ya Yanga, umesema kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar katika
mechi ya juzi, kimewafanya waongeze
nguvu ya mazoezi ili kufanya vema katika michezo ijayo.
Katika
mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba, licha
ya Yanga
kuchezwa kwa juhudi kubwa, ilishindwa kuepuka kichapo cha pili
tangu
kuanza kwa ligi hiyo Septemba 15.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga,
Lawrence Mwalusako, alisema wamepoteza mechi hiyo katika mazingira ya kimchezo.
"Kwa
sasa tunajadili nini kilitufanya tushindwe kufanya vizuri katika mechi za
mikoani, huku tukiongeza nguvu ya kufanya vema katika mechi zijazo, ukizingatia
tuna kocha mpya ambaye ana uwezo mzuri," alisema Mwalusako.
Alisema
kitu muhimu kwao ni kujipanga
vizuri
zaidi kuelekea mechi ya kesho dhidi
ya Toto
Africa ya Mwanza itakayochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.