WACHEZAJI wanne wa mabingwa wa ligi kuu Bara, Simba wakiwemo Nahodha Juma Kaseja,
Mrisho Ngasa, Shomari Kapombe na Mwinyi Kazimoto wanatarajiwa kuonekana katika
nchi mbalimbali duniani baada ya wasifu wao na baadhi ya picha cha michezo yao
kurekodiwa kabla ya kurushwa na kituo cha Televisheni cha SuperSport cha Afrika
Kusini.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga
ameiambia Sports Lady blog kwamba, isema zoezi hilo
limewezeshwa na wadhamini wa timu hiyo kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia
bia ya Kilimanjaro na kuongeza kuwa ni hatua nzuri ya kuelekea mafanikio ya
kupata timu za kucheza nje ya nchi kwa wachezaji hao.
“kama mjuavyo SuperSport inaonekana duniani kote hivyo
wachezaji wetu watapa kuonekana na vilabu mbalimbali na kwa njia hiyo wanaweza
kupata timu za kucheza katika sehemu tofauti duniani,”alisema