MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba
‘Wekundu wa Msimba’ wamezidi kuendeleza kampeni za kutetea taji lao baada
ya kuwatoa nishai maafande wa JKT Oljoro kwa mabao 4-1
katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es
Salaam.
Katika mchezo mabao ya Simba yalifungwa na Amri Kiemba aliyefunga mawili, huku Emmanuel Okwi na Felix Sunzu kila mmoja akipachika moja.
Bao la kufutia machozi la Oljoro lilipachikwa na Paul Nonga.