WAKATI
mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara,
Simba wakishuka katika dimba la Taifa kesho kuwavaa maafande wa JKT Oljoro, mabingwa
hao watamkosa mshambuliaji wao, Mrisho Ngassa.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga
aliiambia Sports Lady Blog kwamba Ngassa atashindwa kushuka
dimbani kutokana na kusumbuliwa na Malaria.
Alisema
mbali na Ngassa, katika mchezo huo pia watawakosa Haruna Shamte, Haruni Chanongo na
Shomari Kapombe ambao wanakabiliwa na majeruhi, huku Amir Maftah ambaye
anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa jumamosi iliyopita walipokwaana na
maafande wa Tanzania Prisons.
“Ukiacha
wachezaji hao, wengine wote waliobaki wako vizuri kabisa na kocha amekiweka
sawa kikosi chake kuhakikisha kinashinda mchezo huo na kuzoa pointi tatu
muhimu,”alisema Kamwaga.
Kamwaga
aliongeza kuwa, katika mchezo huo mshambuliaji wao wa kimataifa Emmanuel
Okwi ambaye alikuwa akitunimikia adhabu ya kukosa mechi tatu anatarajiwa
kuongoza mashambulizi kwa maafande wao hao.
Alisema mchezo
huoutakuwa na ushindani mkubwa kwani Oljoro ni moja ya timu nzuri
zinazoshiriki ligi kuu lakini watahakikisha wanaifunga na kujipatia pointi
tatu.