MABINGWA wa ligi kuu bara Simba wamesema
watatoa tamko la kuushangaza umma wa Watanzania iwapo klabu ya Yanga
haitawarejeshea dola 32,000 walizompatia
wa beki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mbuyu Twite kwa ajili
ya kujisajili.
Twite ambaye alikuwa akiichezea APR ya
Rwanda awali Simba ilimsainisha mkataba wa kuichezea katika msimu huu, kabla ya
Yanga kuingilia na kumsajili kwa dau la dola 50,000.
Kutokana na kitendo hicho, Simba
ilishitaki kwa kamati ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo ilitoa maamuzi ya Septemba 10 na
kuitaka Yanga irejeshe fedha hizo ndani ya siku 21 ambazo zilimalizika jana.
Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba wanailaumu TFF kwa
kutoitendea haki kuhusiana na suala hilo.
“Hiyo ni baada ya kimya kingi tuliandika
barua TFF ili kukumbushia juu ya suala hilo, lakini kuna kiongozi mmoja
alitujibu kwa mdomo kuwa tuandike wenyewe barua Yanga kukumbushia malipo hayo
kitu ambacho hakileti mashiko kabisa,”alisema
Aliongeza kuwa kwa suala hilo wamekaa
kimya la kwa Okwi kufungiwa mechi tatu na kulipa faini walituletea barua haraka bila ya bila kuomba.
Hata hivyo, Yanga kupitia
kwa Katibu wake, Lawrance Mwalusako alisema kwamba suala hilo lipo katika
mpangilio mzuri na kama Twite akicheza kesho dhidi ya Simba ujue wamemalizana na Simba.