KLABU ya Yanga kupitia kwa katibu
wake Mkuu, Lawrance Mwalusako imesema imejipanga vema kuhakisha wanashinda
mchezo huo na kupata pointi tatu.
“Kikubwa ni pointi tatu na wala si mabao
6-0 na kuendelea hata tukishinda bao 1-0 ni ushindi tu ambao utatupatia
pointi”, alisema
Mwalusako aliongeza kwamba kikosi cha
timu hiyo kilichopiga kambi kwenye hoteli ya kimataifa ya Double Tree By Hilton
iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam kipo katika hali nzuri na pamoja na mazoezi
wachezaji wamejengwa vema kisaikolojia.
Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo ni
sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani , huku
watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu watalipa sh. 7,000 ,
wakati watakaokaa viti vya rangi ya
chungwa watalipa Sh. 10,000 , huku VIP C
itakuwa sh. 15,000, VIP B watalipa sh.
20,000 na VIP A watalipa sh. 30,000.