Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura
Kwa vile
msimu huu mdhamini mwenyewe ndiye anayegawa vifaa kwa timu, Kamati ya Ligi
imeagiza Vodacom iandikiwe barua na nakala kwa klabu zote ili kujua timu ambazo
tayari zimekabidhiwa vifaa hivyo zikiwemo logo na siku ambapo timu husika
zilipokea.
Baada ya
majibu ya Vodacom ndipo Kanuni za Ligi Kuu zitakapotumika kutoka adhabu kwa
timu ambazo zitabainika kuwa zilipokea vifaa lakini hazikuvitumia.