KOCHA msaidizi wa timu ysa soka ya Simkbas, Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ amejinasibu timu yake kutibua furahas ya ubingwa wa mahasimu wao Yanga,
katika mchezo wao wa ligi kuu bara utakasopigwa Mei 18 kwenye Uwanjua wa Taifa.
Yanga tayari imetwaa
ubingwa huo ulikuwa ukishikiliwa na Simba
kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo.
Alisema kikosi cha kipo imara kwa mechi hiyo na hivyo Yanga
itarajie kipigo nkitakatifu siku hiyo ambacho kitavuruga shamrashara zao za
kusherehekea ubingwa wa ligi hiyo.
“Tutahakikisha tunakimwagia mchanga kitumbua cha Yanga hivyo
waende kusherehekea ubingwa wao wakiwa wamejifungia ndani kwa aibu ya
kipigo,”alisema
Julio aliongeza kuwa kwa sasa kikosi chake kinaendelea na
mazoezi ya kawaida ya mechi zake zilizosalia kwenye ligi hiyo ambapo kabla ya
kuivaa Yanga, keshokutwa wataikaribisha Mgambo Shooting, mechi itakayopigwa
kwenye uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.
Simba ambayo jana iliibamiza Ruvu Shooting kwa mabao 3-1 kwa
sasa imefikisha pointi 42 ambazo zimeiwezesha kupanda hadi nafasi ya tatu ya
ligi hiyo kutoka ya nne.
Katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.